IEBC YAONYA VIJANA DHIDI KUSHIRIKI VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewataka vijana kujiepusha na uhalifu ikiwaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia vijana kuzua vurugu wakati wa uchuguzi.
Akizungumza wakati wa kikao cha mashauriano na washikadau mbalimbali mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon ameweka wazi kuwa tume hiyo haitasita kuwachukulia hatua za kisheria viongozi hao bila kujali iwapo wapo mamlakani au la.
Kwa upand mwingine katibu mkuu katika wizara ya usalama wa ndani Daktari Reymond Omollo ameahidi kuwa wizara hiyo itashirikiana na tume ya IEBC kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































