NDINDI NYORO ATOA KAULI YAKE DHIDI YA KUPANDA KWA MAFUTA NCHINI
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema ongezeko la bei ya mafuta linaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa wananchi huku akitaka serikali kuweka mikakati ya haraka kupunguza gharama ya maisha kwa Wakenya walioathirika na kupanda kwa gharama za usafiri na bidhaa muhimu nchini
Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari kuhusu suala la mafuta Mbunge huyo ameeleza kuwa hatua ya serikali kutoa ruzuku ya shilingi bilioni tano haitoshi kuleta nafuu inayohitajika kwa wananchi akisisitiza kuwa kuna haja ya kuwepo kwa mpango wa kudumu utakaoleta utulivu wa bei za mafuta nchini.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































