#Athletics #Sports

KIPYEGON KUHAMIA MBIO NDEFU

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon amesema anaanza polepole kuhamia mbio ndefu baada ya kutawala mbio za mita 1500 kwa miaka kadhaa.

Kipyegon ataanza msimu wake wa mwaka 2026 katika mbio za mita 5000 kwenye mashindano ya Diamond League yatakayofanyika mjini Keqiao nchini China siku ya Jumamosi.

Akizungumza kabla ya mashindano hayo, Kipyegon alisema anataka kujaribu uwezo wake katika mbio ndefu zaidi, hatua inayoweza kuashiria mabadiliko mapya katika taaluma yake yenye mafanikio makubwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *