AKONNOR ATAKA GOR MAHIA KUDUMISHA NIDHAMU NA UTULIVU KPL
Kocha mkuu wa Gor Mahia, Charles Akonnor, amewataka wachezaji wake kuwa watulivu, wenye nidhamu na kudhibiti presha kabla ya mechi dhidi ya Murang’a Seal Jumapili katika uwanja wa Nyayo.
Mchezo huo ulihamishwa kutoka Murang’a hadi Nairobi kutokana na changamoto za miundombinu na maandalizi. Gor Mahia wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 65, saba mbele ya AFC Leopards.
Akonnor amesema licha ya presha ya kutwaa ubingwa, wachezaji wake wanapaswa kubaki makini na kucheza kwa umakini hadi dakika ya mwisho.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































