RUTO ANA REKODI ZA KILA MBUNGE, GACHAGUA ADAI.
Kuweni tayari kubeba msalaba wa hongo mliyopokea ili kupitisha hoja ya kunibandua kutoka afisini.
Ndiyo kauli ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini ambako ameibua madai kwamba wabunge na maseneta walihongwa na serikali tendaji ili kupitisha hoja ya kumfurusha afisini.
Gachagua amedai kuwa Rais William Ruto atatumia fursa hiyo kuwashika mateka kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa.
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































