MSHUKIWA WA KIFO CHA RECHAEL ATAENDELEA KUSALIA KOROKORONI KWA SIKU 21
Wachunguzi wa kesi za jinai DCI wanaopeleleza kesi ya mauaji ya mwanamziki Rechael Wandeto wameomba mahakama kuwapa siku 21 kuendelea kumzuilia mshukiwa Josiah Njeru Njiri aliyekamatwa jana kwa kuhusishwa na tukio la kuchomwa moto kwa mwanamziki huyo aliyeaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.
Njiru ambaye ni dereva wa teksi amefikishwa mahakamani hii leo huku uchunguzi wa kubaini kamili mazingira yaliyopelekea kuchomwa kwa mwendazake ukiendelea.
Kukamatwa kwa mshikiwa huyo kunajiri wakati mashirika yakutetea haki za kibinadamu yakionya kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji ya wanawake nchini , Kwa mujibu wa shirika la AMNEST INTERNATIONAL angalau wanawake 8 huuliwa nchini kila wiki huku kati ya wanawake wenye umri wa miaka 18 hadi 35 wakiathirika zaidi.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































