#uncategorized

KENYA YAIMARISHA UKAGUZI WA EBOLA MPAKANI

Serikali ya Kenya imeimarisha uangalizi na ukaguzi katika mpaka wa Busia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo uliosababisha zaidi ya vifo 130.

Serikali imetuma timu ya wahudumu wa afya kuwachunguza wasafiri wanaotoka ukanda wa Maziwa Makuu baada ya taarifa kuwa nchi jirani ya Uganda tayari imeripoti kifo kimoja kinachohusishwa na virusi vya Ebola.

Maafisa wa afya kaunti ya Busia wakiongozwa na Waziri wa Afya wa kaunti hiyo Arthur Odera wamesema hatua hizo zinalenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo nchini kupitia mipaka ya kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *