#Sports

POLICE BULLETS YAPANGA KUIMARISHA KIKOSI KUELEKEA CECAFA

Mwenyekiti wa Kenya Police Bullets Munga Nyale ametaka kikosi hicho kuongezewa nguvu kuelekea michuano ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ukanda wa CECAFA.

Police Bullets walitwaa taji lao la tatu mfululizo la Ligi Kuu ya Wanawake nchini baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Madira Soccer Assassins katika mechi ya mwisho ya msimu uliochezwa kwenye uwanja wa Police Sacco.

Timu hiyo ilimaliza msimu ikiwa na alama 52, alama nane mbele ya Ulinzi Starlets huku mashindano ya CECAFA yakitarajiwa kuandaliwa mjini Kigali kati ya Agosti 22 na Septemba 6 mwaka 2026.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *