AFYA YA UMMA NAIROBI YATAHADHARISHA MGOMO
Maafisa wa afya ya umma jijini Nairobi wameituhumu bodi ya huduma ya kaunti kwa kuajiri maafisa wasio na sifa kushughulikia usalama wa chakula na uthibitisho wa afya.
Kupitia Chama cha Maafisa wa Afya ya Mazingira na Afya ya Umma, Katibu Mkuu wa chama Brown Ashira amesema hatua hiyo inakiuka sheria za afya ya umma na kanuni za usimamizi wa wataalamu wa afya.
Chama hicho kimeonya kuwa udhaifu katika usimamizi unaweza kuhatarisha usalama wa chakula na maji jijini, hali inayoweza kusababisha milipuko ya magonjwa ya kuambukiza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































