#Local News

WADAU WAPINGA BAADHI YA VIPENGELE VYA MSWADA WA FEDHA 2026

Wadau wanaoshiriki vikao vya maoni kuhusu Mswada wa Fedha 2026 wameilaumu serikali kwa kushindwa kurekebisha viwango vya ushuru wa mishahara maarufu kama PAYE pamoja na kuanzisha ushuru mpya kwa miamala ya fedha kupitia simu.

Wakizungumza mbele ya Kamati ya Fedha na Mipango ya Bunge la Taifa la Kenya, Taasisi ya Wahasibu Walioidhinishwa Kenya (ICPAK) pamoja na Muungano wa Mabenki nchini wamesema ongezeko la ushuru linaendelea kudhoofisha uwezo wa sekta ya huduma kuzalisha nafasi mpya za ajira.

Wadau hao wameonya kuwa ushuru mwingi unaweza kuongeza mzigo wa maisha kwa wananchi na kuathiri ukuaji wa uchumi nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *