#Football #Sports

APS BOMET YAICHAPA BANDARI KWA MABAO MAWILI

Mshambuliaji Hillary Juma aliiongoza APS Bomet FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bandari FC katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kwale.

Mechi hiyo ndiyo pekee ya ligi kuu kuchezwa baada ya FKF kuahirisha michezo mingine kutokana na changamoto za usafiri zilizosababishwa na vurugu za sekta ya uchukuzi.

Juma alifunga bao la kwanza dakika ya 69 baada ya kuwatoka mabeki wa Bandari kabla ya APS Bomet kuthibitisha ushindi huo kwa bao la pili kipindi cha pili.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *