WACHEZAJI WAPYA WAPATA NAFASI KWENYE LIONESSES
Mchezaji Maria Gorette wa Guins Queens anaongoza kundi la wachezaji wanane wapya walioitwa kwenye kikosi cha Kenya Lionesses kwa mashindano ya Rugby Africa Women’s Cup yatakayofanyika katika viwanja vya RFUEA Grounds jijini Nairobi kuanzia leo hadi tarehe 31 mwezi huu.
Kocha Simon Odongo amesema kujumuishwa kwa wachezaji hao wapya kunaonyesha ukuaji wa vipaji kutoka mashindano ya humu nchini na mifumo ya maendeleo ya mchezo huo.
Kenya itaanza kampeni yake dhidi ya Uganda Mei 23 kabla ya kukutana na Madagascar na baadaye mabingwa watetezi Afrika Kusini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































