GACHAGUA AILAUMU SERIKALI KUCHOCHEA GHASIA NCHINI
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ameisuta serikali kwa kuchochea hasira za wananchi kupitia namna inavyoshughulikia uchumi, sera za sekta ya usafiri na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Akizungumza akiwa nchini Uingereeza Gachagua alijibu kauli za Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar, aliyekuwa amehoji sababu za hasira za wananchi dhidi ya Rais William Ruto.
Gachagua amesema viongozi wa serikali wenyewe wanachangia kuongeza mivutano ya kisiasa nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































