MBADI AKOSOA WANAOPINGA MSWADA WA FEDHA
Waziri wa Fedha John Mbadi amemkosoa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i pamoja na viongozi wengine wa upinzani wanaotaka Mswada wa Fedha 2026 ukataliwe.
Mbadi amesema viongozi wanaowataka Wakenya kupinga mswada huo wanapaswa kwanza kueleza vipengele wanavyopinga badala ya kutoa matamshi ya kisiasa ya jumla.
Mbadi amesema ni makosa kuwahamasisha wananchi kuandamana dhidi ya mswada bila kutoa mapendekezo mbadala au kueleza kasoro zilizopo ndani yake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































