MAKAMISHNA WA NCIC WAAPISHWA RASMI NA KOOME
Hatimaye makamishna wapya walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu katika tume ya uwiano na utangamano kitaifa NCIC wameapishwa.
Rais wa idara ya mahakama nchini jaji mkuu Martha Koome ameapisha makamishna hao katika shuguli iliyofanyika katika mjengo ya upeo wa mahakama hapa nchini.
Makamishna hao wanaongozwa na mwenyekiti wao mpya Daktari Kefa Nyamea Omae, ni Makamishna Josphine Kirion,Joseph keunguyo, Jackson Swadi Kedogo, Samuel Mwachiru Mwawasi, Irene Chepoisho Tule, Hassan Ahmed na Jerusha Mwathime Michael.
Akizungumza katika hafla hiyo Koome amewataka kulihudumia Taifa kwa kulifanya swala la uwiano kapaumbele na kuliunganisha taifa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































