BUNGE LAKUBALI MAPENDEKEZO YA NDINDI NYORO KUHUSU MAFUTA
Bunge la Taifa limekubali kuyazingatia mapendekezo ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro yanayolenga kupunguza bei ya mafuta nchini.
Kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Bajeti ya Bunge, Bunge limethibitisha kupokea barua ya Nyoro ya Mei 15 yenye mapendekezo ya marekebisho ya sheria yanayolenga kupunguza gharama ya dizeli kwa angalau shilingi 54 kwa lita.
Hatua hiyo imejiri wakati serikali ikiendelea na mazungumzo na wadau wa sekta ya uchukuzi kufuatia mgomo wa matatu uliosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































