BIASHARA HARAMU YA NYAMA YA PUNDA YAENDELEA KAJIADO
Biashara haramu ya nyama na ngozi za punda imeendelea kushamiri nchini licha ya serikali kupiga marufuku uchinjaji wa kibiashara wa wanyama hao mwaka 2020.
Katika eneo la Kimuka, wakazi walinasa lori lililokuwa likisafirisha nyama inayoshukiwa kuwa ya punda pamoja na ngozi zake kabla ya kuwashambulia watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kajiado Magharibi Maureen Jepkemboi amesema ripoti ya maafisa wa mifugo ilithibitisha kuwa lori hilo lilikuwa limebeba nyama ya punda 30 pamoja na ngozi zake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































