RONALDO ASHINDA TAJI LAKE LA KWANZA SAUDI ARABIA
Cristiano Ronaldo ameshinda taji lake la kwanza la ligi nchini Saudi Arabia baada ya kuiongoza Al-Nassr kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Damac FC katika mechi ya mwisho ya msimu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 alifunga mabao mawili muhimu katika ushindi huo uliowapa taji la muda mrefu ambalo alikuwa akilikosa katika misimu miwili iliyopita licha ya kufika fainali mara kadhaa.
Ronaldo, ambaye alijiunga na Al-Nassr mwaka 2023, amekuwa na takwimu bora binafsi akishinda kiatu cha dhahabu msimu wa 2023/24 kwa mabao 35 kabla ya kufunga mabao 25 katika msimu wa 2024/25, akithibitisha ubora wake licha ya ushindani mkali katika ligi hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































