ELIUD KIPCHOGE KUSHIRIKI CAPE TOWN MARATHON
Eliud Kipchoge anatarajiwa kushiriki mbio za Cape Town Marathon Jumapili nchini Afrika Kusini katika harakati za kuongeza historia nyingine katika taaluma yake.
Bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki amewasili mjini Cape Town tayari kuipa mbio hiyo hadhi zaidi huku waandalizi wakisaka kuitambua kama mbio za kwanza Afrika kuingia kwenye mashindano ya Abbott World Marathon Majors.
Mashindano hayo pia ni sehemu ya mpango wa Kipchoge wa kukimbia katika mabara yote saba duniani ndani ya miaka miwili ijayo ili kuhamasisha maisha yenye afya kupitia riadha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































