EPRA YAHAKIKISHA HAKUNA UPUNGUFU WA MAFUTA
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli EPRA imesema Kenya ina akiba ya mafuta ya kutosha kudumu angalau mwezi mmoja licha ya changamoto za usambazaji duniani.
Mkurugenzi wa mafuta na gesi Edward Kinyua amesema nchi ina akiba ya dizeli na petroli ya kutosha pamoja na meli kadhaa zilizoko tayari kushusha shehena katika bandari ya Mombasa.
Ameongeza kuwa pia kuna meli nyingine za mafuta zilizoko pwani ya Mombasa zikisubiri kushusha mzigo ili kuimarisha usambazaji nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































