KAMATI YA BUNGE YACHUNGUZA UHABA WA MAFUTA
Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu Kawi na Petroli imezuru maghala ya mafuta ya Kenya Pipeline katika jiji la Nairobi kuchunguza kiini cha uhaba wa mafuta unaoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Ziara hiyo inalenga kubaini changamoto katika usambazaji na uhifadhi wa mafuta pamoja na hatua zilizochukuliwa kushughulikia hali hiyo.
Kamati hiyo imeahidi kuwasilisha ripoti yao baada ya uchunguzi ili kusaidia kupata suluhu ya kudumu kwa tatizo la upatikanaji wa mafuta nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































