#Local News

“UJUMBE UMEFIKA!” RAILA AKUBALI SHUTUMA ZA WAKENYA

Kinara wa Azimio Raila Odinga amekiri kwamba Wakenya hawataki mazungumzo ya kitaifa ambayo yeye kwa Pamoja na Rais William Ruto waliitisha hapo jana kujadili masuala yanayolikumba taifa.

Kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa X baada ya mkutano na viongozi wa ODM akiwemo Seneta Edwin Sifuna wa Nairobi, Eddie Oktch wa Migori na Crystal Asige, Raila amesema nikimknukuu, “Nimeambiwa na hawa viongozi kwamba mmesema hamtaki handshake. Ujumbe umefika.” Mwisho wa nukuu.

Raila amezungumza siku moja baada ya kuwahimiza vijana washiriki mazungumzo ya kitaifa kujadili masuala ya kitaifa ukiwemo uksoefu wa ajira.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

“UJUMBE UMEFIKA!” RAILA AKUBALI SHUTUMA ZA WAKENYA

WAKAZI WAMWUA MSHUKIWA KOROKORONI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *