#Local News

BAADHI YA VIONGOZI WA ODM WAUNGA MKONO SERIKALI JUMUISHI

Baadhi ya viongozi wa Chama cha ODM wanaounga mkono serikali jumuishi wamesema wataendelea kushirikiana na serikali baada ya kuwa muda mrefu katika upinzani.

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama Gladys Wanga wamesema ushirikiano na serikali utasaidia maeneo yao kupata maendeleo na kunufaika zaidi.

Wamewahimiza wafuasi wao kuunga mkono serikali huku baadhi wakipendekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga maeneo ya kisiasa maarufu kama zoning.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *