#Local News

MABADILIKO KATIKA ULINZI WA RAIS RUTO BAADA YA HITILAFU YA KIUSALAMA

Huduma ya Polisi imefanya mabadiliko katika kikosi cha usalama wa Rais William Ruto baada ya hitilafu ya kiusalama iliyotokea Kaunti ya Kilifi

Katika tukio hilo, kijana mmoja alivunja ulinzi wa rais na kufika karibu na jukwaa wakati Rais alipokuwa akihutubia wananchi.

Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais Noah Maiyo amehamishwa kwenda makao makuu ya polisi, huku William Sawe akiteuliwa kuongoza kikosi hicho mara moja.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *