MWILI WA MWANAMKE WAPATIKANA KWENYE MFUKO WA PLASTIKI EMBAKASI
Maafisa wa upelelezi katika eneo la Embakasi wanafanya uchunguzi baada ya kiwiliwili cha mwanamke kupatikana ndani ya mfuko wa plastiki kando ya Barabara ya North Airport karibu na uzio wa uwanja wa ndege.
Polisi walisema mwili huo uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana karibu na kituo cha mafuta katika eneo hilo, huku kichwa cha marehemu kikikosekana.
Kamanda wa Polisi wa Nairobi Issa Mohamud amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































