BUNGE LAPINGA TAARIFA ZA USHURU KWA ARDHI YA UMILIKI WA KUDUMU
Bunge la Kitaifa limekanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni kuwa Mswada wa Fedha 2026 unapendekeza Wakenya kulipa kodi ya kila mwaka kwa ardhi ya umiliki wa kudumu.
Bunge hilo limesema madai hayo ni ya kupotosha na yanalenga kuwachanganya wananchi kuhusu yaliyomo kwenye mswada huo.
Limefafanua kuwa Mswada wa Fedha 2026 hauna kipengele chochote kinachohusu ushuru wa ardhi, umiliki wa kudumu wala kubadilisha ardhi hiyo kuwa ya kukodisha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































