VIONGOZI WA KENYA KWANZA WAONYESHA IMANI KWA RUTO 2027
Baadhi ya viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza wameeleza imani kuwa Rais William Ruto atapata muhula wa pili kutokana na rekodi yake ya maendeleo na juhudi za kuunganisha taifa.
Wakizungumza katika eneo bunge la Turbo, Viongozi hao Wamedai kuwa viongozi wa upinzani wanaendeleza siasa za mgawanyiko badala ya kuangazia maendeleo ya wananchi.
Aidha wamemtetea Rais kuhusiana na swala zima la mafuta nchini wakisema kuwa ni tatizo la dunia zima wala si la taifa hili pekee.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































