#Football #Sports

GOR MAHIA WATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA FKF

Gor Mahia wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF msimu wa 2025/26 baada ya AFC Leopards kufungwa mabao 2-1 na APS Bomet.

K’Ogalo wameweka rekodi mpya kwa kutwaa taji lao la 22 licha ya kutocheza mechi yao dhidi ya Mara Sugar iliyositishwa kutokana na mzozo wa uwanja.

Matokeo hayo yaliiacha AFC Leopards nyuma kwa alama nne huku ikiwa imesalia mechi moja pekee, na hivyo kuthibitisha Gor Mahia kuwa mabingwa rasmi wa ligi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *