ULINZI STARS WAPANIA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA
Kocha wa Ulinzi Stars Mulinge Ndeto amesema timu hiyo itaendelea kupigania kusalia katika Ligi Kuu ya SportPesa hadi mwisho wa msimu.
Kauli hiyo imejiri baada ya Ulinzi Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mathare United, ushindi uliowapa matumaini mapya ya kuepuka kushuka daraja.
Timu hiyo sasa iko nafasi ya 15 ikiwa na alama 35 huku zikiwa zimesalia mechi mbili muhimu kabla ya msimu kumalizika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































