KENYA YASHINDWA KUTAMBA CAPE TOWN MARATHON
Mashindano ya Sanlam Cape Town Marathon yalikuwa magumu kwa wanariadha wa Kenya huku nchi ikipata nafasi moja pekee ya jukwaani katika mbio za wanaume na wanawake.
Kalipus Lomwai ndiye aliyekuwa Mkenya pekee kumaliza katika tatu bora baada ya kushika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:05:06 katika mbio za wanaume.
Mbio hizo zilitawaliwa na wanariadha wa Ethiopia wakiongozwa na Mohamed Esa aliyeshinda kwa rekodi mpya ya mashindano, huku marathon hiyo ikiweka historia kama mbio za kasi zaidi kuwahi kuandaliwa barani Afrika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































