#Business

EPRA YAAHIRISHA MIKUTANO YA HADHARA KUHUSU MAPENDEKEZO MAPYA YA USHURU WA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imeahirisha vikao vya mashauriano vya umma nchini kote kuhusu mapendekezo ya ombi la bei ya reja reja ya umeme kwa mara ya tano kwa Udhibiti wa Ushuru wa mwaka wa kifedha 2026/27 hadi 2028/29.

Katika notisi ya umma ambayo imetolewa, EPRA imetangaza kwamba mabaraza hayo, ambayo yalipangwa kuanza leo hii sasa yatafanyika mwezi Juni.

Kulingana na mdhibiti ni kwamba mashauriano hayo sasa yatafanywa katika kambi mbalimbali za kiuchumi za kikanda kati ya Juni 15 na Juni 24 mwaka huu. Mikutano hiyo inatarajiwa kutoa fursa kwa wadau wa sekta mbalimbali na wananchi kutoa maoni yao kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya bei ya umeme.

Ratiba iliyorekebishwa iliyotolewa na EPRA inaashiria kuwa kongamano hilo litaandaliwa katika miji mbali mbali ikiwa ni Pamoja na Kisumu, Eldoret, Nakuru, Nyeri, Nairobi, Garissa na Mombasa.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *