SERIKALI, UPINZANI WALUMBANA KUHUSU 2022
Viongozi wa upinzani na serikali wameendelea kulaumiana kuhusu jinsi kampeni za aliyekuwa mwaniaji wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kupitia tiketi ya Azimio Raila Odinga zilivyoshuhudiwa, chama cha Jubilee kikimtetea kinara wake Uhuru Kenyatta dhidi ya madai kwamba hakutoa fedha za kuwalipa maajenti.
Kwenye kikao na wanahabari, Jubilee ikiongozwa na katibu mkuu Jeremiah Kioni na Waziri wa zamani wa usalama Fred Matiang’i, wamekariri madai ya katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna kwamba fedha hizo zilifujwa na aliyekuwa ajenti mkuu wa Azimio Junet Mohammed.
Wameikosoa serikali kuhusiana na mashambulizi dhidi ya Kenyatta.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































