KSSSA: LAISER HILL KUVAANA NA FSK KWENYE VIKAPU
Mabingwa watetezi wa mchezo wa vikapu wa wavulana katika michezo ya shule za upili Laiser Hill, watachuana na Friends School Kamusinga hii leo katika semi fainali za mashindano ya shule za upili kwa muhula wa kwanza jijini Kisumu.
Laiser Hill walipata ushindi mwembamba dhidi ya Lukenya School wa 71-69 na kuweka miadi ya kumenyana na FSK katika juhudi za kutetea taji hilo.
Kwa upande wao, Kamusinga walimaliza wa pili katika Pool yao baada ya kulazwa 74-72 na limbukeni St. Mary’s Yala ambao nao watamenyana na Lukenya School katika semi fainali nyingine.
Katika safu ya akina dada, bingwa mara tatu Butere Girls watavaana na Barchondo Girls kwenye fainali moja, huku mabingwa wa zamani Kaya Tiwi wakimaliza udhia na St. Brigid’s Kiminini katika semi fainali nyingine.
Katika ulingo wa raga, Kisii School watafufua uhasama wao na St. Mary’s Yala kwenye raga ya 15 aside hii leo kwenye semi fainali.
Semi fainali nyingine itakutanisha Upper Hill na mabingwa wa zamani Kakamega High katika uwanja wa Jomo Kenyatta.
Kisii walijitangaza kama miamba baada ya kushinda mechi zote za ufunguzi.
Kwa upande wa akina dada, mabingwa wa national 7s Kinale, watamenyana na Mbagathi huku St. Joseph’s Girls wakichuana na Mwira.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































