WANAOHODHI MAFUTA CHUMA MOTONI
Mamlaka inayodhibiti ushindani wa kibiashara nchini imezionya kampuni za uuzaji wa mafuta nchini dhidi ya kuficha mafuta hayo kwa matarajio ya kuuza kwa bei ya juu kutokana na uhaba unaoendelea kuripotiwa nchini.
Kupitia taarifa, mamlaka hiyo imesema ina ufahamu kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu uwepo wa mafuta ya petroli, diseli, mafuta ya taa na ndege kote nchini, pamoja na taarifa ambazo zimetolewa na wawakilishi wa kampuni hizo.
Imekariri kuwa mafuta ni bidhaa muhimu na kwamba wanaoficha au kuongeza bei kiholela watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































