#uncategorized

BUNGE LA KITAIFA KUREJELEA VIKAO VYAKE KWA KUANDAA VIKAO MAALUM KUJADILI MSWADA WA FEDHA MWAKA 2024

Bunge la kitaifa leo hii linatarajiwa kurejelea vikao vyake kwa kuandaa vikao maalum kujadili mswada wa fedha mwaka 2024.


Vikao hivi vinatarajiwa kuangazia yaliyomo katika mswada huo ulioratibu kwa mapana mzigo Zaidi wa kodi kwa wakenya ambao wamesakamwa na gharama ya juu ya Maisha.


Mswada huu mbali na kupendekeza bei ya mkate kuongezwa . Mswada huu pia unapendekeza kuondolewa kwa huduma za benki, kodi Zaidi ikiongezwa katika sekta ya boda boda serikali ikilenga kukusanya Zaidi ya shilingi bilioni 320 za kodi mwaka huu.


Marekebisho yamependekezwa kuhusu ulinzi wa data ili kuipa nafasi mamlaka ya kodi KRA kupata data za kibinafsi za wakenya na biashara zao.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *