#Local News

AULIWA BAADA YA KUMUUA MKEWE KWA SABABU YA SHILINGI 30

Maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa cha kusikitisha ambapo mzee wa miaka 60 anadaiwa kumdunga kisu na kumuua mkewe katika mzozo wa Sh30 katika kijiji kimoja Kaunti ya Siaya.

Mwanamume huyo aliyetambulika kama Ben Odweso baadaye aliuawa na kundi la watu waliojawa na gathabu baada ya kisa hicho katika kijiji cha Nyalula.

Alidaiwa kumdunga kisu na kumuua mkewe Pamela Anyango mwenye umri wa miaka 55 jana Jumapili kufuatia kutoelewana kuhusu Sh30.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *