#Local News

MAANDAMANO YASHUHUDIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI

Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini yamefanyka katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Roysambu, nyeri, Nyahururu miongoni mwa maeneo mengine.

Waandamanaji hao wamefunga baadhi ya barabara na kuchoma magurudumu hali ilyolemaza shuguli za uchukuzi katika maeneo hayo huku polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwatanya waandamanaji hao waliokuwa wamefunga sehemu  ya barabra  kuu ya Thika.

Katika jiji la Nairobi hofu kuhusu maandamano hayo ilisababisha taharuki miongoni mwa wakazi katikabaadhi ya maeneo huku wengine wakiripoti changamoto za usafiri  kufungwa kwa baadhi ya barabara  na kupanda kwa nauli.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *