#Sports

CHELSEA KUKUTANA NA PSG KWENYE FAINALI

Paris St-Germain iliibomoa Real Madrid na kuandaa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa dhidi ya Chelsea Jumapili.

Mchezo huu wa nusu-fainali kwenye Uwanja wa MetLife ulikamilika kama shindano ndani ya dakika 24 huku washindi wa Ligi ya Mabingwa waliporarua timu ya Uhispania.

Fabian Ruiz alifunga bao la kwanza dakika ya sita kufuatia makosa makubwa kutoka kwa beki wa Real Raul Asencio – baada ya mwamuzi kuruhusu mchezo uendelee kufuatia Thibaut Courtois kumchezea vibaya Ousmane Dembele.

Winga Mfaransa, Dembele alikimbia dakika tatu baadaye na kumaliza kwa utulivu baada ya mpira uliopigwa vibaya na Antonio Rudiger.

PSG waliingia Kombe la Dunia la Vilabu mwishoni mwa kampeni ambapo walishinda Ligue 1 na Kombe la Ufaransa kabla ya kuwalaza Inter Milan 5-0 kwenye fainali na kushinda UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Iwapo watapata uwezo wa kushinda Chelsea katika fainali Jumapili kwenye Uwanja wa MetLife huko New Jersey utamaanisha PSG kushinda kila mashindano ambayo wameshiriki msimu huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

CHELSEA KUKUTANA NA PSG KWENYE FAINALI

ULINZI STARS YAPATA MWENYEKITI MPYA

CHELSEA KUKUTANA NA PSG KWENYE FAINALI

TUKO TAYARI KWA CHAN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *