#Local News

SERIKALI YATANGAZA MAJARIBIO YA CHANJO

Serikali kuu imeratibiwa kuanzisha majaribio ya chanjo zilizotengenezwa humu nchini katika kipindi cha miaka 2 ijayo, kwenye zoezi litakalohakikisha kuwa taifa linajitegemea katika masuala ya chanjo.

Zoezi hilo litaendeshwa kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia itakayotoa shilingi bilioni 8, magonjwa yanayolengwa yakiwa ni kichomi yaani pneumonia na homa ya matumbo yaani typhoid miongoni mwa watoto.

Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa kituo cha chanjo cha Kenya BioVax Daktari Charles Githinji, chanjo aina 3 dhidi ya ugonjwa huo zitatolewa kufikia mwaka wa 2027.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI YATANGAZA MAJARIBIO YA CHANJO

BALAA YA DHARURA AMREF

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *