OMANYALA SPRINT CLUB YAZINDULIWA ISINYA KUINUA RIADHA YAMBIO ZA KASI
Riadha ya mbio za kasi nchini Kenya imepata msukumo mkubwa kufuatia uzinduzi wa
Omanyala Sprint Club mjini Isinya, Kaunti ya Kajiado.
Klabu hiyo yenye malengo makubwa ilizinduliwa Jumatano katika Shule ya Merishaw,
Isinya, ikiwa ni hatua muhimu katika kulea na kukuza kizazi kipya cha wanariadha wa mbio
fupi.
Mpango huo unaendeshwa kwa nguzo tatu kuu, huku ukuzaji wa vipaji vya mbio za kasi
ukiwa kitovu chake. Unatokana na imani kuwa kila chipukizi wa mbio anastahili fursa sawa
ya kufikia uwezo wake kamili.
Mpango huu, unanuia kubaini, kukuza na kuwalea wanariadha wachanga kwa kuwaandalia
njia zilizo wazi kutoka riadha za shule hadi mashindano ya kiwango cha juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































