ULINZI STARS WAWATIMUA MAKOCHA OCHOLLA, ONYISO
Klabu ya Ulinzi Stars imemsimamisha kazi kwa muda kocha mkuu Stephen Ocholla na msaidizi wake Francis Onyiso, kutokana na matokeo duni ambayo yameshuhudia klabu hiyo ikicheza mechi 9 bila ushindi.
Matokeo hayo duni yamewaacha wanajeshi hao wakishikilia nafasi ya pili kutoka chini mwa jedwali, wakiwa na pointi 19 pekee baada ya mechi 24.
Kichapo cha hivi punde kimekuwa mabao 3-1 dhidi ya Gor Mahia Jumapili, na kuongeza masaibu ya klabu hiyo ambayo sasa inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja.
Ocholla alirejea kwenye kikosi hicho Oktoba mwaka jana kwa mara ya pili, na kuchukua mahali pa Dunstan Nyaundo, ambaye alikuwa na wakati mgumu kuwaimarisha wanajeshi hao mwanzoni mwa msimu.
Kwa sasa vijana hao watanolewa na mchezaji wa zamani wa Harambee Stars James Mulinge Ndeto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































