#Local News

MAFURIKO YAWASUMBUA WAKAZI ELDORET

Mamia ya wakazi wa jiji la Eldoret wameshindwa kutoka majumbani mwao kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali.

Mto Sosiani umefurika na kuelekeza maji katika maeneo ya makazi, hali iliyosababisha uharibifu na kuhatarisha maisha ya wakazi.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na mtaa wa Elgon View ambako wakazi wanakabiliana na athari za mafuriko hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *