#Local News

RUTO AONGOZA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NAIROBI

Rais William Ruto pamoja na Rais wa Msumbiji Daniel Chapo wameongoza kongamano la uwekezaji katika hoteli moja hapa jijini Nairobi.

Zaidi ya kampuni 20 zimekubali kuwekeza zaidi ya dola bilioni 2.9 katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo afya, kilimo na madini, huku kaunti kama Kilifi, Nairobi, Tana River na Kitui zikitajwa kunufaika.

Rais Ruto ametumia fursa hiyo kuwashukuru wawekezaji akisema Kenya iko tayari kwa uwekezaji, akiongeza kuwa raia wake wana uwezo na fursa bora za kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *