#Local News

MIMI KATIBU WA OBURU? MTANISAMEHE- SIFUNA

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, amekariri msimamo wake kwamba hatahudumu kwenye wadhifa huo chini ya kinara wa sasa wa chama hicho Oburu Oginga, kwa misingi kwamba Oburu hana haiba hitajika ya kukiongoza chama hicho.

Kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa kaunti ya Mombasa, Sifuna aliyekuwa ameandamana na viongozi wamengine wanaoegemea mrengo wake wa Linda Mwananchi, amewakosoa viongozi wa Linda Ground kwa madai ya kupotoka kutoka kwenye msimamo wa ODM kuwatetea wananchi.

Wamedai kwamba ukanda wa pwami umeachwa nyuma licha ya uwakilishi serikalini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *