#Rugby #Sports

SHUJAA WAREJEA NCHINI KUTOKA BRAZIL

Timu ya taifa ya raga ya wanaume ya wachezaji 7 kila upande, Shujaa, imerejea nchini kutoka Sao Paulo Brazil ambako walitia for a katika mkondo wa mwisho wa HSBC SVNS II, na kufuzu awamu ya mabingwa.

Shujaa ilimaliza katika nafasi ya 3 katika mikondo miwili ya kwanza iliyoandaliwa Kenya na Uruguay, kabla ya kuhitimisha kampeni yao katika nafasi ya pili wikendi iliyopita.

Kwa sasa, vijana hao wa Kelvin Wambua wana fursa ya kuwania nafasi ya kupandishwa daraja na kushiriki HSBC Division 1 msimu ujao.

Katika kipute cha World Rugby Championship, Shujaa watamenyana kwenye mikondo mitatu vile vile ambako ni Hong Kong Uchina, Valladolid nchini Uhispania na kisha Bordeaux nchini Ufaransa.

 Kwenye mkondo wa kwanza, Shujaa wamejumuishwa katika Group C, kundi linalojumuisha New Zealand, Australia na Marekani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *