#Sports #Volleyball

VOLIBOLI: TIMU ZA KENYA ZAPANGIWA MAKUNDI MAZITO AFRIKA

Timu za juu za mpira wa wavu wa wanawake nchini Kenya zimepata wapinzani wao kufuatia droo ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika mjini Cairo, Misri.

Kenya Pipeline wamewekwa Kundi B wakikutana na timu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Ghana na Burundi, huku DCI Queens wakipangwa Kundi C pamoja na timu kutoka Tunisia, Nigeria, Uganda na Kongo.

Katika Kundi D, KCB watamenyana na timu kutoka Cameroon, Nigeria na Ushelisheli, huku timu za Kenya zikilenga kurejesha ubingwa wa bara uliotwaliwa mara ya mwisho na KCB mwaka 2022.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *