#Local News

DUALE AONYA HOSPITALI KUHUSU ULAGHAI WA SHA

Waziri wa Afya Aden Duale ameonya vituo vya afya vinavyoshiriki katika mpango wa mamlaka ya afya ya jamii akisema vitakavyohusika na vitendo vya ulaghai vitafutiwa mikataba mara moja

Akizungumza katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Bungoma Duale amesema mageuzi ya kidijitali yanayoendelea yanalenga kuimarisha uwazi uwajibikaji na utoaji wa huduma bora huku akiwataka wasimamizi wa vituo hivyo kufuata kikamilifu mfumo mpya

Ameongeza kuwa baadhi ya hospitali zinachunguzwa kwa tuhuma za ukiukaji wa taratibu na kusisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kulinda rasilimali za umma na kudumisha imani ya wananchi katika sekta ya afya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *