#Local News

RUTO AZUA VICHEKO BUNGENI TANZANIA

Rais William Ruto amewachekesha wabunge wa Tanzania baada ya kueleza kwa utani sababu ya kutumia lugha ya Kiingereza badala ya Kiswahili wakati wa hotuba yake.

Akihutubia bunge hilo, Ruto alitoa maelezo ya kihistoria kwa kuhusu Kiswahili kabla ya kuamua kutumia Kiingereza, akisema hataki kukosea katika matumizi ya lugha hiyo.

Kauli hiyo ilizua vicheko miongoni mwa wabunge, huku ziara yake rasmi nchini humo ikilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Nairobi na Dodoma.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

RUTO AZUA VICHEKO BUNGENI TANZANIA

USIKU MKUBWA WA ARSENAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *