#Local News

KINDIKI ASUTA VIONGOZI  WA SIASA WENYE MATAMSHI MABAYA

Naibu wa Rais Kithure Kindiki amejitenga na baadhi ya matamshi ya viongozi wa chama cha UDA kuwa wanalenga kuhitilafiana na matokeo ya Urais mwaka wa 2027 ili kumpa ushindi Rais William Ruto iwapo atapata kura chache katika uchaguzi mkuu ujao.

Akijibu kauli ya viongozi  hao akiwemo  naibu wa gavana wa kaunti ya kakamega Ayubu Savula, Kindiki amesema ni bora viongozi wa mirengo yote kufanya siasa komavu  ili kuimarisha amani nchini hata baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Aidha amesema kuwa ana imani kuwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC  itafanya uchaguzi mkuu ujao kwa huru na haki.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *