MAANDAMANO YASHUHUDIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI
Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini yamefanyka katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Roysambu, nyeri, Nyahururu miongoni mwa maeneo mengine.
Waandamanaji hao wamefunga baadhi ya barabara na kuchoma magurudumu hali ilyolemaza shuguli za uchukuzi katika maeneo hayo huku polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwatanya waandamanaji hao waliokuwa wamefunga sehemu ya barabra kuu ya Thika.
Katika jiji la Nairobi hofu kuhusu maandamano hayo ilisababisha taharuki miongoni mwa wakazi katikabaadhi ya maeneo huku wengine wakiripoti changamoto za usafiri kufungwa kwa baadhi ya barabara na kupanda kwa nauli.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































